Search This Blog

Wednesday, November 20, 2019

Lukaku aongoza waliopiga nyingi wakiwa na miaka 26

LONDON ,ENGLAND . STRAIKA wa Kibelgiji, Romelu Lukaku amekuwa akifurahia maisha yake matamu kwenye kikosi cha Inter Milan na sasa amefunga mabao 246 akiwa na umri wa miaka 26.

Hii hapa orodha ya wanasoka waliofunga mabao mengi zaidi wakiwa na umri wa miaka 26.

5. Harry Kane - mabao 218

Anatajwa mmoja wa mastraika bora kabisa duniani kwa sasa. Harry Kane anashika namba tano na mabao yake 218 kwa wakali waliofunga mabao mengi wakati anatimiza umri wa miaka 26. Straika huyo wa Tottenham Hotspur ni mchezaji muhimu kwenye klabu yake na timu ya taifa na umri wake wa sasa unampa nafasi ya kwenda kuvunja rekodi nyingi za mabao huko England.

4. Luis Suarez - mabao 223

Mshindi mara mbili wa Kiatu cha Dhahabu cha Ulaya, alishinda pia tuzo hiyo kwenye Eredivise, Ligi Kuu England na La Liga, ambako inafahamika kama Pichichi.

Advertisement

Straika Luis Suarez alikuwa kwenye ubora mkubwa wa kutupia mabao alipokuwa Liverpool kipindi hicho umri wake ukiwa miaka 26. Staa huyo wakati anafika umri huo alikuwa amefunga mabao 223.

3. Wayne Rooney - mabao 227

Kinara wa mabao wa muda wote wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Wayne Rooney, alianza kucheza soka lake la kulipwa akiwa na umri wa miaka 16 tu na hadi anafikisha umri wa miaka 26, staa huyo alikuwa amefunga mabao 227 kwenye michuano yote aliyocheza kwa ngazi ya klabu na timu ya taifa. Ulaya alicheza timu mbili, Everton na Man United.

2. Robert Lewandowski - mabao 231

Kinara wa mabao wa wachezaji wa kigeni kwenye Bundesliga, Robert Lewandowski atakumbukwa kama mmoja wa washambuliaji bora kabisa kuwahi kutokea duniani.

Lewandowski hafundishwi kufunga kama ilivyo tu kwa samaki asivyofundishwa kuogelea. Staa huyo wakati anafikisha umri wa miaka 26 alikuwa ameshatikisa nyavu mara 231, uhodari ambao amekuwa akiendelea nao hadi sasa.

1. Romelu Lukaku - mabao 246

Huyu ndiye mtu aliyefunga mabao mengi zaidi wakati anafikisha umri wa miaka 26. Straika huyo wa zamani wa Manchester United, anayekipiga kwenye kikosi cha Inter Milan kwa sasa, Romelu amekuwa moto kwenye kutupia na kufunga mabao 246. Lukaku ameshafunga mabao 52 kwenye soka la kimataifa na huenda akafunga mara nyingi zaidi.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...