Search This Blog

Friday, November 15, 2019

Klopp afunguka kila kitu kuhusu Zlatan

LIVERPOOL, ENGLAND . LISEMWALO ni kwamba supastaa Zlatan Ibrahimovic huenda akarudi tena kwenye Ligi Kuu England baada ya timu kadhaa kuonekana kuhitaji saini yake huku Liverpool wakibanwa na jambo moja tu kunasa saini yake.
Kocha Jurgen Klopp amefichua kwamba wangetamani sana kupata saini ya mshambuliaji huyo, lakini kuna kitu kinawabana katika kuinasa huduma yake.
Zlatan, 38, amefichua wazi kwamba anaachana na LA Galaxy na hivyo mpango wake ni kurudi Ulaya, ambako huko Italia amekuwa akihusishwa na AC Milan, huku kuna wakati jina lake lilihusishwa pia na uwezekano wa kuhamia Hispania.
Klopp alisema sababu moja kubwa inayowafanya washindwe kumsajili Zlatan, akisema: “Kama ingekuwa hajawahi kuichezea Manchester United huko nyuma, tungeshawishika kumsajili."
"Lakini, sasa sidhani kama atahitaji kuja kucheza hapa kwetu. Sisi ni timu yenye ushindani zaidi…"
Ibrahimovic wakati wale aliokuwa Old Trafford ulikuwa safi ambapo alishinda mataji matatu likiwamo la Kombe la Ligi, ambapo alifunga bao la ushindi kwenye fainali dhidi ya Southampton. Baada ya Man United alienda zake Marekani, ambako alifunga mabao 30 kwenye mechi 29 alizocheza katika ligi ya MLS.
"Nilichokisema si kwamba namkosea heshima Zlatan, namheshimu san, nampenda na napenda anavyojiamini na ni mtu anayeburudisha," alisema Klopp.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...