Search This Blog

Saturday, November 30, 2019

Klopp aambiwa anajisumbua kwa Mbappe, hampati

MONACO, UFARANSA . ALIYEKUWA makamu wa rais wa AS Monaco, Vadim Vasilyev amewaambia Liverpool wasijisumbue kabisa kuhusu kuhangaika kumsajili straika wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe kwa sababu hawawezi kumpata.
Liverpool wamekuwa wakihusishwa na staa huyo mshindi wa Kombe la Dunia, lakini Vasilyev alisema Mbappe mpango wake wote ni kwenda Real Madrid na hilo halina mjadala ni suala la muda tu.
Vasilyev, ambaye ndiye aliyemuuza Mbappe kwenda PSG, aliliambia Le Parisien: "Kylian atakwenda Real Madrid, sijui ni lini, lakini hilo halizuiliki.
"Klabu hiyo ni muhimu sana kwenye maisha yake. Madrid walileta ofa tamu zaidi kuliko PSG mwaka 2017, lakini aliniambia kwamba anadhani ilikuwa mapema sana kuondoka Ufaransa na Paris ndio nyumbani kwake.
"Alitaka kuwa mchezaji mahiri Ufaransa kwamba apate muda wa kuonyesha kiwango chake kwao kwanza kabla ya mengi na hapo Kylian alionyesha kuwa na akili kubwa. Kwa sasa ni mchezaji bora kabisa Ufaransa na PSG wana pesa za kutosha kuendelea kumbakiza kwenye timu yao."
Baada ya kusikia kwamba Mbappe mwenyewe yupo tayari kuachana na PSG, Liverpool inayonolewa na Mjerumani, Jurgen Klopp ilionekana kuwa na dhamira ya dhati ya kunasa huduma ya supastaa huyo wa kimataifa wa Ufaransa.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...