Search This Blog
Sunday, November 24, 2019
Hili Hapa Jibu la Ommy Dimpoz kwa TID Baada ya Kuambiwa Ajui Kuimba
Msanii Ommy Dimpoz amesema hana uhakika na kile alichokipost msanii TID, baada ya kumuorodhesha katika oroddha ya wasanii watano wabovu wa Bongo Fleva ambapo TID alimuweka Ommy Dimpoz nafasi ya pili.
Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital Ommy Dimpoz amesema hana uhakika kama ni TID kama ndiyo alipost kweli katika mtandao wa kijamii wa Twitter,
"Kwanza mimi sipo Twitter kwa sababu akaunti yangu watu waliidukua taKribani mwaka sasa ila naishughulikia kuirudisha, Pili nilitumiwa tu hiyo "list" lakini mwisho wa siku sina uhakika kama ni TID mwenyewe, hata kama yeye ni kaka yetu kila mtu ana maoni yake na mtazamo wake" amesema
"Mwisho wa siku tupo katika nchi ya huru kila mtu anaweza kujisikia kwa kile anachokifanya, nilichukulia kawaida tu ila kwangu mimi ukiniuliza kuhusu TID nitakwambia ni mmoja wa wasanii bora waliowahi kutokea kwenye BongoFleva" ameongeza
Aidha Ommy Dimpoz amewajibu waliombeza kwamba hajastahili kuchukua tuzo za AFRIMMA kama msanii bora wa kiume Afrika Mashariki kwa kusema, "Mimi niliwekwa katika category, nikaomba kura kwa sababu walioniweka waliona nastahili kwahiyo hizo zote nichangamoto tu kwangu hakuna jipya"
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment