Search This Blog

Saturday, November 23, 2019

Emery akataa pesa za usajili

LONDON, ENGLAND . STAA wa zamani wa Arsenal, Lee Dixon amewataka mabosi wa timu hiyo kamwe wasithubutu kumpa pesa za usajili kocha Unai Emery wakati wa dirisha la uhamisho wa Januari litakapofunguliwa.
Arsenal amepita kwenye nyakati ngumu msimu huu na jambo hilo linamfanya kocha Emery kuwa kwenye presha kubwa ya kutafuta matokeo. Kabla ya mechi ya jana, Arsenal ilikuwa haijashinda mchezo wowote katika mechi nne zilizopita na kwamba walikuwa wameshinda mechi nne tu katika 12 walizokuwa wachezaji kwenye Ligi Kuu England.
Januari ingeweza kuwa njema kwa Emery kutokana na kupata nafasi ya kuboresha kikosi chake ili kiwe na nguvu ya kuchuana kuwania Top Four, lakini Dixon anaamini kwamba kuendelea kutumia pesa chini ya kocha huyo ni uamuzi wa hovyo.
“Sina maana kwamba nataka Emery afukuzwe kazi. Ninachokiamini ni kwamba kocha anahitaji miaka kama miwili hivi kuweka mambo sawa, lakini huyu Emery naona kama anaishi kwenye ndoto vile," alisema Dixon.
“Emery yupo kwenye presha kubwa, hivi anaweza kumaliza matatizo ya Arsenal kwa kusajili Januari? Mabosi wanaona nini? Bila ya shaka wanapaswa kulitazama hilo kwa tahadhali.”
Arsenal mechi zake nne zilizofuatia, alikuwa akicheza na timu za chini, ikiwamo ile ya jana Jumamosi waliyomenyana na Southampton na baada ya hapo watakipiga na Norwich City, Brighton na West Ham United, hivyo kocha Emery anapaswa kuchanga vyema karata zake kwenye mechi hizo ili kuokoa kibarua chake.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...