Search This Blog
Saturday, October 19, 2019
Wazazi wanaowashawishi watoto wao kufanya vibaya kwenye mitihani kushitakiwa
Wazazi na walezi wenye watoto wanaosoma wameonywa kuhujumu ndoto za watoto kwa kuwashawishi kufanya vibaya katika mitihani yao ya mwisho kwa lengo la kuwafanya watoto hao kutoendelea na masomo yao ya baadae na badala yake kuwatumia katika mambo yao ikiwemo kuwaozesha na wengine kuwafanyisha kazi za kilimo na ufugaji.
Onyo hilo limetolewa na mdau wa maendeleo na mkurugenzi wa kampuni za Boma Security Company Ltd, Evance Kamenge alipokuwa akiwahutubia wazazi,walezi, walimu pamoja na wanafunzi kwenye mahafari ya darasa la saba katika shule ya msingi Nyabihanga iliyopo wilayani Missenyi mkoani Kagera.
“Serikali inatoa pesa nyingi kuwasomesha watoto wenu na pesa hizo zinatolewa Zaidi ya shilingi bilioni 23 kila mwezi za elimu bure, cha ajabu wapo wazazi na walezi wachache wenye malengo mabaya na kuwashawishi watoto wao kufanya vizuri kwenye mitihani yao ili wasifahulu, mimi niseme tu kwa mzazi yeyote atakayebainika nitachukua jukumu la kumshitaki katika vyombo vya sharia kwa hujuma hizo.” Amesema Kamenge.
Zaidi ya wanafunzi 610 katika kata ya Kasambya wilayani Missenyi wamefanya mtihani wa darasa la saba, wanafunzi 585 wamefahulu mtihani huo katika matokeo yaliyotangazwa siku chache zilizopita ambapo wazazi wametakiwa kujiandaa ili kuhakikisha watoto hao wanakwenda sekondari,
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment