Search This Blog
Wednesday, October 30, 2019
Wananchi wa Kisarawe wahakikishiwa huduma ya Maji ndani ya siku tatu
Kufikia mapema wiki ijayo, Wakazi wa mji mdogo wa Kisarawe wanaondoka na na adha ya maji ya muda mrefu baada ya ujenzi wa mradi wa Kisarawe kukamilika kwa asilimia 99.
Hatua hiyo imefikiwa, baada ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) kukamilisha ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa Lita Milioni 6 kukamilika.
Mradi huo wenye thamani ya Bilioni 10.6 uliojengwa kwa fedha za ndani za Dawasa unaotoa maji kutoka Tanki la maji la Kibamba hadi Kisarawe.
Kuanza kwa mradi huo kutawanufaisha wananchi wengi zaidi na maunganisho mapya 1000 watakao unganishwa maji kwa mkopo na kulipa ndani ya mwaka mmoja.
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameupongeza uongozi wa Dawasa kwa jitihada kubwa walizozifanya ndani ya muda mfupi kwa kuhakikisha maji yanafika katika mji mdogo wa Kisarawe.
“Naupongeza uongozi wa Dawasa, Mwenyekiti, Mkurugenzi na watendaji wengine kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuhakikisha wanajenga mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya Bilioni 10.6 kwa fedha za ndani na kuleta maji kwenye Mji mdogo wa Kisarawe.”
“Mradi huu umechukua muda mfupi sana, na ndani ya siku tatu hizi nataka kuhakikisha wananchi wanapata maji kesho nitaandamana na baadhi ya viongozi kuelekea Kibamba maji yanakoanzia ili kujionea mwenyewe,” amesema Aweso.
Amesema, kuna changamoto ya umeme ambapo amewahakikishia wananchi wa Kisarawe mita itapatikana na maji yataanza kuingia kwenye tanki na huduma ya maji itaanza.
Kaimu Mkurugenzi Uwekezaji Miradi Dawasa ,Mhandisi Ramadhani Mtindasi amesema mradi wa maji Kisarawe umekamilika kwa asilimia 99 na kazi iliyobaki ni ndogo sana na Dawasa wanaendelea kuhakikisha ndani ya muda mfupi maji yanafika kama agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli alilolitoa.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya Kisarawe, Jokate Mwengelo amewataka wananchi wa mji mdogo wa Kisarawe kuwa na subira ndani ya siku chache wataanza kupata maji safi na salama.
”Niwatake na kuwaomba wananchi wa Kisarwe na wale walio nje ya mji huu kwamba kwa sasa nawakaribisha kuja kuwekeza kwenye Mji mdogo wa Kisarawe, maji yatakayokuwa hapa yanatosheleza mahitaji ya wakazi wote ambapo kwa sasa ni Lita Milion 1.2 zinazohitajika ila Dawasa wametuletea Lita Milion 6,” amesema.
Mji mdogo wa Kisarawe unapata maji kutoka Mtambo wa Ruvu Juu na umeweza kufanikishwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja ukitekelezwa na Dawasa ambapo kufikia Septemba Mwaka huu Mji huo umekabidhiwa rasmi kwa Mamlaka hiyo.
Mbali na mradi huo, Naibu ameweza pia kutembelea shule aliyosoma ya Pugu Sekondari, Shule aliyofundisha Kisarawe pamoja na Kisima alichokuwa anatumia kwa ajili ya matumizi ya maji sambamba na mradi wa maji wa Jet Buza wenye thamani ya Bilion 2 unaotarajia kuanza hivi karibuni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment