Search This Blog

Tuesday, October 8, 2019

Vikwazo 174 vya biashara EAC vimeondolewa kwa Wafanyabiashara


Jumla ya vikwazo 174 sawa na asilimia 75 vimeondolewa ili kurahisisha ufanyaji biashara kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo sasa itawezesha kuwepo kwa biashara kubwa baina ya nchi hizo.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika Ufunguzi wa Mkutano kati ya Wafanyabiashara na Kamati ya Taifa inayoshughulikia vikwazo vya biashara, Mkurugenzi Msaidizi wa  Idara ya Mtangamano wa Biashara, Bi. Sekela Mwaisela alisema kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na kanda zingine kuna sheria ambazo zinazingitia biashara.

"Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Ibara ya 13(1) Itifaki ya Umoja wa Forodha ya Biashara pamoja na Ibara ya 6 ya Itifaki ya Biashara kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zaKusini mwa Afrika (SADC) zinazitaka Nchi Wanachama kuondoa vikwazo vya zamani ili kuwezesha biashara kwa wafanyabiashara," Alisema Mwaisela.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...