Search This Blog

Tuesday, October 29, 2019

Umoja wa Mataifa wataja majanga yanayoikumba Afrika


Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) limeangazia majanga ambayo yanakumba bara la Afrika miongoni mwao ukame nchini Zambia na mafuriko ya maji nchini Somalia na Sudan Kusini.

Katibu Mkuu wa shirika hilo Antonio Guterres alisema kuwa Sudan Kusini imeathirika zaidi kutokana na mafuriko tangu mwezi wa Julai. Takriban watu 900,000 wameathirika nchini humo ikiwemo wakimbizi wa ndani na wenyeji.

Zambia kwa upande mwingine imekumbwa na janga la ukame kutokana na ukosefu wa mvua, hali ambayo haijashuhudiwa tangu mwaka wa 1981.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...