Search This Blog

Tuesday, October 1, 2019

TRA yaweka rekodi ya makusanyo septemba


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekusanya mapato ya Serikali jumla ya shilingi 1.767 trilioni katika kipindi cha mwezi Septemba pekee.

Makusanyo haya, ambayo ni sawa na ufanisi wa asilimia 97.20 ya lengo la kukusanya la jumla ya kiasi cha shilingi 1.817 trilioni katika kipindi cha Septemba 2019 hayajawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa TRA kwa kulinganisha na makusanyo ya Septemba 2018.

Kwa mujibu wa taarifa ya TRA kwa vyombo vya habari, ufanisi huo wa Septemba 2019 ni mwendelezo wa ongezeko la makusanyo tangu mwaka wa fedha wa 2019/2020 ulioaza Julai 2019.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...