Search This Blog

Wednesday, October 23, 2019

Sheria ya ndoa kubadilishwa


Mahakama ya rufani imetupa rufaa ya Serikali ya Tanzania iliyokuwa ikipinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyobatilisha vifungu vya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 vinavyoruhusu mtoto wa kike chini ya umri wa miaka 18 kuolewa.

Hukumu hiyo imetolewa baada ya mahakama hiyo kukubaliana na hoja za jopo la mawakili wa mjibu rufaa lililoongozwa na Mpale Mpoki, Jebra Kambole (aliyeshinda kesi ya msingi), Alex Mgongolwa na Fulgence Massawe.

Serikali ilikata rufaa kupinga hukumu hiyo iliyotokana na  kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na mwanaharakati na mkurugenzi wa shirika lisilo la Kiserikali la Msichana Initiative, Rebeca Gyumi.

Jopo la majaji watatu waliosikiliza rufaa hiyo lililoongozwa na Augustine Mwarija (kiongozi wa jopo), Winfrida Korosso na Dk. Mary Lavira, limeithibitisha hukumu hiyo ya Mahakama Kuu, baada ya kutupilia mbali hoja zote za rufaa ya Serikali kuwa hazikuwa na mashiko.

Mahakama ya rufani katika hukumu yake iliyosomwa leo Jumatano Oktoba 23, 2019 na naibu msajili, Fussi imesema kuwa Mahakama Kuu ilikuwa sahihi kuamua kuwa vifungu hivyo ni vya kibaguzi kati ya mtoto wa kike na wa kiume na havina manufaa yoyote kwa mtoto wa kike.

”Hivyo tunaitupilia mbali rufaa hii yote kutokana na kutokuwa na mashiko,” amesema Fussi akinukuu hukumu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...