Search This Blog
Tuesday, October 1, 2019
Rais Magufuli amuapisha Mkurugenzi NEC na Balozi na Mkuu wa Itifaki Wizara ya Mambo ya Nje
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Dkt. Wilson Mahera Charles kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Kabla ya uteuzi na uapisho huo Dkt. Wilson Mahera Charles alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha. Dkt. Wilson Mahera Charles amechukua nafasi ya Bw. Athuman Kihamia ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Kanali Wilbert Augustine Ibuge kuwa Balozi na Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocal) wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Balozi Kanali Ibuge amechukua nafasi ya Mhe. Balozi Grace A. Martin ambaye atapangiwa majukumu mengine ya Kibalozi. Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Oktoba 01,2019.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...



No comments:
Post a Comment