Search This Blog
Thursday, October 3, 2019
Prince Harry na Meghan walipokutana na mama Graca Machel
Mjane wa hayati Nelson Mandela, Graca Machel amesema amejisikia fahari kukutana na mtawala wa Sussex Prince Harry na mkewe Meghan Markle nchini Afrika Kusini na kusisitiza kuwa anauhakika katika siku za mbeleni watafanya kazi pamoja.
Prince Harry na mkewe walifanikiwa kukutana na mke huyo wa hayati Mandela mwenye miaka 73 jijini Johannesburg katika siku ya mwisho ya ziara yao ya Afrika ambapo mbali na kutembelea Afrika Kusini, Harry pia alifanya ziara ya pekee yake katika nchi za Angola, Botswana na Malawi huku akimuacha mkewe Meghan na mtoto wao Archie jijini humo.
Mbali na kukutana na Graca Machel, wawili hao pia walipata wasaa wa kukutana na Rais wa nchi hiyo, Cyril Ramaphosa na mkewe kabla ya kuondoka nchini humo baada ya kumaliza ziara yao ya siku kumi barani Afrika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...



No comments:
Post a Comment