Search This Blog
Saturday, October 5, 2019
Nikupongeze Mh Rais kwa Kuungana na RC Chalamila
Habarini za asubuhi wanajamvi...
Hakika kutoka ndani ya moyo wangu naomba kumpongeza Mh Rais kwa kwenda sambamba na RC Chalamila kuwachapa viboko wanafunzi waliochoma bweni kisa wamenyang'nywa simu..
Kwanza kuwa na simu ili hali wewe ni mwanafunzi ni kosa la kwanza na kuchoma bweni ni kosa la pili,
Kabla Mh Rais hajampongeza RC Chalamila Mimi nilimpongeza kimoyomoyo,kizazi cha sasa cha hovyo sana,tusipoenda nao kwa style hii walimu watapata tabu sana,
Kitu ambacho vijana hawa bado hawajakielewa Nchi imebadilika sana,wasifikiri tupo awamu ya nne ya mchezo mchezo hii ni awamu ya tano ya kazi tu hatuna muda na mambo ya kijinga kama haya eti unachoma bweni kisa kunyang'anywa simu wakati tayari umevunja sheria kumiliki simu shuleni?
Nakupongeza sana Mh Rais kwa kuliunga mkono hili,
Tukiendelea kulea mambo ya kijinga kama haya tutashindwa kupiga hatua...
Hongera Mh Rais
Hongera RC Chalamila
By Huko Kwenu Vipi/JF
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment