Search This Blog

Tuesday, October 29, 2019

Ndugu Waanza Kutambua Maiti ya Ajali ya Gari iliyoanguka Katika Daraja Handeni


Miili ya watu waliopoteza maisha kutokana na ajali iliyotokea katika Wilaya ya Handeni mkoani Tanga  imeanza kutambuliwa na ndugu zao.

Gari waliyokuwa wanasafiria lilianguka katika daraja  lililokatika kutokana na mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha mkoani humo.

Jitihada mbalimbali zinaendelea ili kuhakikisha barabara ya Kilindi Handeni inafunguka na kikosi jeshi cha 121 kutoka Ngerengere kimeanza kuleta vifaa kwa ajili ya ujenzi wa madaraja yaliyokatika.

Wakati huo huo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe amesema kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na ajali hiyo imeongezeka na kufikia watu 12 baada ya kupatikana kwa miili miwili.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...