Search This Blog

Monday, October 28, 2019

Naibu Spika aongoza Kamati ya Maazimio Chama cha Wabunge Wanawake wa Mabunge Jumuiya ya Madola


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, ameongoza Kamati ya Maazimio ya Semina ya Wajumbe wa Chama cha Wabunge Wanawake wa Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika uliofanyika Mkoani Arusha.

Katika Semina hiyo iliyofunguliwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan jana Oktoba 27, 2019 imepitisha maazimio mbalimbali yakiwemo:

Mosi; Mabunge Wanachama wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika yatunge na kuhakikisha zinatelekezwa sheria zitakazohakikisha vyama vya siasa vinazingatia usawa katika nafasi za uongozi; sheria zitakazozuia ama kuadhibu makosa yanayohusiana na ukatili na unyanyasaji wa wanawake kipindi chote cha uchaguzi.

Pili; Serikali za nchi husika zihakikishe kunakuwa na mtaala wa elimu kuhusu jinsia.

Tatu; Serikali husika na wadau wengine kuhakikisha inatolewa elimu juu ya masuala ya ushiriki wa wanawake katika uchaguzi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...