Search This Blog

Saturday, October 26, 2019

Mondi Amdekeza Tanasha kama yai!

STAA grade one wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ humuambii kitu kwa mama wa mtoto wake mpya, Tanasha Donna Oketch kwa namna anavyomdekeza kama yai.



Tanasha kwa sasa anaishi maisha baabkubwa kwa kuwa baba wa mtoto wake huyo anamjali ile mbaya. Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ya familia ya Diamond au Mondi, Tanasha kuwa na jamaa huyo kama baba wa mtoto wake ni jambo la kifahari kwake hivyo anadeka kadiri atakavyo.



Baada ya kumzalia Mondi, sasa Tanasha ambaye ni mtangazaji na msanii wa muziki wa Kizazi Kipya anajiona kama malkia.



Kuthibitisha hilo, mapema wiki hii alitupia picha kwenye Insta Story akiringishia simu ya bei mbaya aliyonunuliwa na Mondi kama zawadi. Kufuatia zawadi hiyo, Tanasha alishindwa kujizuia na kujikuta akishukuru mno kwa zawadi hiyo;

“Nina furaha sana sasa hivi, asante Diamond Platinum kwa upendo wako kwangu.”

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...