Wimbo wa Kijiwe Nongwa ni moja kati ya nyimbo ambazo zimetoka hivi karibuni na kukamata watu kwelikweli, habari ikufikie kwamba mpaka muda ambao naandika makala haya Kijiwe Nongwa umetazamwa na watu wasioupungua Milioni 1.
Wimbo huu wa Roma na Stamina ambao wamemshirikisha Nay wa Mitego ambao kwenye mtandao wa YouTube umepandishwa Septemba 20, mwaka huu, unayo mistari mingi mitamu na ya kusisimua lakini makala haya yanakuchambulia ile mistari ambayo ina nongwa kwelikweli, ujumbe wake unatupa vijembe kwa watu wengine bila kuusahau ule uliotoa majibu kuhusu madai ya muda mrefu kuhusu ndoa zao kuvunjika!
- MAREHEMU WALIMSEMA MNYONYAJI…KWANI MUZIKI UNA MAZIWA…
- BABU WA LOLIONDO YULE MWENYE BLICHI LA KIKONGO… SASA UCHAGUZI UMEKARIBIA AMERUDI CHAMA TAWALA…
- ALIKUJA KAMA MASII, TUKAMCHANGIA SADAKA…NA BADO WAKAMLAZA MUUMINI KIFO CHA MENDE.
- ALIYEOKOTA ALMASI MCHANGANI ALIKUWA MISS TANZANIA, NA ALIYEKUJA INUNUA DUKANI NI MGANDA ALIYEKUWA NA NIA…
Dongo kwa msanii mkubwa wa Bongo Fleva ambaye anasifika kwa kuwamaliza warembo na mwishoni Roma amemchana kuwa msanii huyo ni mnyanyasaji wa kijinsia.
- NIAMBIE MAANA YA TFF…
- VIPI DADA YETU WA IGUNGA, MH SIMUONI UDANGANI… FUNDI YULE FUNDI GEREJI CHAWA SI KAMTEKA BIBIE NA WAMEFUNGUA MGAHAWA YANI WOTE MAMA N’TILIE.
- SA SIKIZA MAN, VIPI SHEMU MAMA IVAN? TUPOTUPO TU ILA SI KAMA ZAMANI… NAWE VIPIB KWANI, MBONA WIFE SIMUONI NYUMBANI? CHILL MAN, SINA MAJIBU DEAL DONE.
- BONGO BWANA NDIO NCHI INAYOSAPOTI SANA UJINGA…

No comments:
Post a Comment