Search This Blog
Friday, October 4, 2019
Magufuli Amnyooshea Kidole Mwele Malecela Asema Alitumiwa na Mabeberu Kutangaza Ugonjwa 'Hewa' wa Zika
Akielezea ni kwa namna gani humpelekea kufanya kazi hadi usiku Rais Magufuli amesema katika vita hasa ya kiuchumi adui mbaya zaidi hutoka ndani kwa maana ndiye huwa kiungo wa maadui wa nje.
Ametolea mfano wa aliyekuwa Mkurugenzi wa NIMR TANZANIA Bi Mwele Malecela alilazimika kumfuta kazi baada ya yeye kutoa taarifa za uongo kwamba wakati ule kulikuwa na ugonjwa wa Zika ilhali haikuwa kweli.'Je huo ugonjwa wa Zika ulionekana tena!?'alihoji Mheshimiwa Rais!
Amesema hali hiyo ya Mwele kuutangazia uongo Ulimwengu kuhusu uwepo wa zika Nchini Tanzania ilimkwaza sana na dhahili alionekana kutumiwa na washindani wa vita ya kiuchumi na Nchi yetu.
'Na ndiyo maana baada ya kumfuta kazi wiki moja baadae waliomtumia walimpa kibarua kingine'alisema Mheshimiwa Rais.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment