Search This Blog

Wednesday, October 2, 2019

KRC Genk ya Samatta yapata pointi moja kwa Napoli


Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta leo ameiongoza timu yake ya KRC Genk kama nahodha katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Napoli ya Italia.

Mchezo huo uliopigwa kwenye Dimba la Luminus nchini Ubelgiji, umemalizika kwa suluhu, kila timu ikishindwa kutikisa nyavu za mwenzake.

Huo ni mchezo wa pili kwa Samatta kucheza kwenye Ligi ya Mabingwa barani Ulaya akiwa ni Mtanzania pekee kuwahi kucheza hiyo.

Matokeo hayo yanaifanya Genk kupata pointi moja pekee katika michezo miwili ambayo imeshacheza hadi sasa ikitoka kuchapowa 6-2 na Salzburg katika mchezo wa kwanza, huku Napoli wakifikisha pointi 4.

Mchezo mwingine wa kundi hilo la E unapigwa kuanzia saa 4:00 usiku kati ya Liverpool na Salzburg kwenye Dimba la Anfield, Liverpool wakiwa wanaingia na kumbukumbu za kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Napoli kwenye mchezo wa kwanza.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...