Juhudi za uokozi zimeshika kasi kuwafikia watu waliokwama kwenye maeneo yaliyokumbwa na mafuriko baada ya kimbunga kikali kuyapiga maeneo kadhaa ya Japan, ikiwemo mji mkuu, Tokyo.
Kimbunga Hagibis ambacho kimesababisha mvua kubwa na upepo mkali kiliwasili kusini mwa mji wa Tokyo jana Jumamosi kabla ya kuelekea upande wa kaskazini.
Kulingana na Shirika la Habari la Japan, kimbunga hicho tayari kimesababisha vifo vya watu 11 na zaidi ya majeruhi 100, huku watu wengine zaidi ya 17 bado hawajulikani waliko.
Picha za vidio zimeonesha helikopta ikiwaokoa watu katika eneo la Nagano ambalo limefurika maji baada ya kingo za mto Chikuma kupasuka.
Kiasi polisi na wanajeshi 17,000 wamewekwa tayari kwa ajili ya shughuli za uokozi huku mamlaka nchini Japan zikionya kuwa hatari ya kutokea maporomoko ya udongo bado ni kubwa.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment