Search This Blog

Sunday, October 27, 2019

Kifo cha Mwenyekiti wa Kijiji cha mtoa machozi Mbunge


Kifo cha Mwenyekiti mstaafu wa Kijiji Cha Musini na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Kata ya Sepuka Mkoani Singida,  Mzee Jumanne Njoghomi kimeleta simanzi kubwa kwa watu waliokuwa wakimfahamu na kumtoa machozi Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu wakati wa kumuombea dua marehemu.

Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu, akilia wakati wa dua ya kumuombea Mzee Jumanne Njoghomi aliyefariki Oktoba 22 mwaka huu nyumbani kwake Kata ya Sepuka mkoani Singida
Wengine walioshindwa kujizuia na kuanza kulia kufuatia kifo cha mwenyekiti huyo ni pamoja na wazee,vijana,wanawake na hali hiyo imetokana na uchapaji kazi, ukarimu na upendo aliokuwa nao kiongozi huyo kwa wananchi.

Mbunge Kingu akimuongelea marehemu katika dua hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki alisema kifo chake kimewagusa watu wengi pamoja na yeye kwani alikuwa ni mshauri wake kwa mambo mengi.

“Huyu mzee kwangu alikuwa ni baba na mshauri wangu kwa kweli nimepata pigo sana nashindwa namna ya kumzungumzia” alisema Kingu huku akitokwa machozi.

Mkazi wa kata hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Lissu alisema hakika kila mtu atavuna alichokipanda akiwa hapa duniani kwani mzee Njoghomi alipanda mema na yameonekana baada ya kifo chake hivyo watu tuliopo baki duniani hatuna budi kujichunguza na kubadilika kwa kutenda mema ya kumpendeza mwenyezi mungu.

Ahmed Shabani akizungumza katika dua hiyo alisema ni wakati wa kila mtu kubadilika na  kuachana na vitendo vinavyomchukiza mwenyezi mungu kama kugombea ardhi,uchoyo,wizi,dhuluma na kujivuna kutokana na utajiri na kueleza kuwa vyote hivyo tutaviacha hapa duniani.

Mwalimu wa Msikiti wa Mtunduruni uliopo Singida mjini, Hamis Ndiba alisema alichopanda marehemu enzi za uhai wake ndicho kinachojidhihirisha baada ya kifo chake kwani alikuwa mnyenyekevu kwa watu wote na msuluhishi wa migogoro mbalimbali katika mkoa huo.

”Marehemu enzi za uhai wake hakumbagua mtu awe mkristo au muislam aliwasikiliza na kuwasaidia ikiwa ni pamoja na kuwajulia hali wagonjwa na kuhudhuria misibani hakika tumempoteza mtu ambaye alikuwa muhimu sana kwetu” alisema Ndiba.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Sepuka, Juma Mghenyi alisema marehemu enzi za uhai wake aliwahi kuwa mwenyekiti wa Kitongoji cha Musini Magharibi kwa miaka 15 na mwenyekiti wa Kijiji cha Musini miaka 15 na mpaka anafikwa na mauti alikuwa ni mjumbe wa kamati ya siasa wa kata hiyo..

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...