Search This Blog
Tuesday, October 1, 2019
Kampeni kuhamasisha uwekaji akiba yazinduliwa
Katika harakati za kuhakikisha jamii ya Watanzania, hasa wanaoishi vijijini wanajenga utamaduni wa kujiwekea akiba, na kufanikisha malengo yao ya muda mfupi na mrefu, Benki ya NBC leo imezindua kampeni maalum itakayodumu kwa miezi sita inayofahamika kwa jina la 'Ibuka Kidedea na NBC'.
Kaimu Mkurugenzi wateja wa Rejareja wa Benki ya NBC Benjamin Nkaka alisema hayo wakati wa warsha fupi ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
“Kampeni hiyo inalenga kuleta mabadiliko kwenye mtazamo wa uhifadhi wa akiba miongoni wa watanzania kutoka kuhifadhi pesa majumbani na badala yake wazihifadhi kupitia benki hiyo huku wakifurahia faida,”
“Ni wakati muafaka sasa kwa watanzania mmoja mmoja au vikundi kuacha kuhifadhi fedha zao kwenye vibubu au namna nyingine yoyote ile majumbani mwao kwa kuwa njia hizo si salama kwao na kiuchumi pia na badala yake wanaweza kuhifadhi pesa zao kupitia akaunti ya Malengo ya NBC ambayo inawahakikishia usalama wa fedha zao huku pia wakifurahia faida zinazotolewa na benki’’ Alisema.
Alizitaja faida zitokanazo na akaunti hiyo ambazo mbali na kuokoa pesa za mteja, pia inaweza kubadilika kuwa amana kulingana na mapato ya mteja. Pia inatoa fursa kwa mteja kuweza kuweka akiba hiyo kupitia mashine za kuwekea fedha (ATM) za benki hiyo zinazopatikana kote nchini, kwenye matawi na kupitia mawakala wa huduka za benki hiyo.
“Habari njema zaidi ni kuwa hakutakuwa na makato ya mwezi huku pia mteja akipata riba ya hadi kufikia asilimia 7 kwa mwezi,’’ aliongeza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment