Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo amewapongeza waandishi wa habari kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuhabarisha Wananchi kuhusu masuala ya sekta ya elimu na Serikali kwa ujumla.
Dkt. Leonard Akwilapo ameyasema hayo wakati wa kikao kati ya wahariri wa vyombo vya mbalimbali vya habari na wizara hiyo ambapo alielezea kiwango cha elimu nchini na kusema kinaendelea vizuri na hatua mbalimbali zinafanyika kuiboresha sekta ya elimu.
Ameongeza kuwa Dira ya wizara ni kuwa na Mtanzania aliyeelimika na mwenye maarifa, stadi, umahiri, uwezo na mitazamo chanya ili kuweza kuchangia katika kuleta maendeleo ya Taifa.
Dkt. Akwilapo ameongeza kuwa jumla ya shilingi Bil. 93.8 zimetumika kuimarisha miundombinu katika shule 588 za msingi na sekondari zikiwemo shule kongwe. ambapo serikali imeongeza mikopo ya elimu ya juu kutoka Tzs Bil. 424.7 mwaka 2018/2019 hadi Tzs Bil. 450 mwaka 2019/2020.
Akielezea kuhusu makusanyo ya madeni ya wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu amesema yameongezeka kutoka Tzs Bil. 21.1
mwaka 2014/2015 hadi Tzs Bil. 183.2 mwaka 2018/2019 ambapo wizara inafanya mapitio ya sera ya elimu ya mwaka 2014 ili kuifanyia maboresho na kuendana na wakati.
Amewaasa viongozi wa sekta ya elimu kushirikiana na waandishi wa habari kwa uwazi ili wananchi wapate taarifa za sekta ya elimu zenye usahihi na kwa wakati.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment