Search This Blog
Monday, October 7, 2019
Anayedaiwa kumbaka mwanae hukumu kutolewa Ijumaa hii
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imepanga kutoa hukumu Oktoba 11, mwaka huu, dhidi ya kigogo wa Taasisi ya Utafiti na Udhibiti wa Viuatilifu katika ukanda wa Kitropikali ya (TPRI), Aresteric Silayo, anayedaiwa kumbaka mwanawe wa kike (11).
Akizungumza Mahakamani hapo, Hakimu Mkazi Aziza Temu, aliyepewa mamlaka na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kusikiliza rufani ya kesi hiyo, alisema amesikiliza hoja za rufani hiyo za pande zote mbili.
"Baada ya kuwasikiliza upande wa utetezi na Jamuhuri, hukumu nitatoa Oktoba 11, mwaka huu," alisema.
Kabla ya hakimu Aziza kupanga tarehe hiyo, alimsikiliza Wakili wa Serikali, Azael Mwiteni, ambaye aliomba mahakama hiyo kutengua uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ya kumwachia huru mtuhumiwa huyo.
"Mheshimiwa naomba utengue uamuzi wa kumwachia huru mtuhumiwa huyu na kuzingatia ushahidi wa mtoto na mashahidi wote waliofika mahakamani hapa kutoa ushahidi unaofanana na usio na mashaka," aliiambia mahakama.
Alieleza ushahidi wa mtoto (jina tunalo) unaonyesha baba (mtuhumiwa) alimbaka mwanawe kwani mtoto aliweza kumweleza Mwalimu shuleni, mahakamani na pia cheti cha daktari aliyemchunguza amethibitisha mtoto huyo kubakwa.
"Kutokana na ushahidi uliotolewa Mheshimiwa utaona utakapopitia jalada hili kuwa mtoto ameeleza bila kubadili maneno, naomba mtie hatiani mshtakiwa na kumpa adhabu stahiki kulingana na kitendo alichokifanya kwa mwanawe.”
Naye Wakili wa Utetezi, John Materu, alidai hoja za Wakili wa Serikali hazina mashiko, kwani mahakama ilimwachia huru baada ya kuona ushahidi uliotolewa mahakamani ulikuwa wa shaka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment