Search This Blog
Saturday, September 14, 2019
Waziri Wa Afya: Hakuna Ugonjwa wa Ebola Tanzania
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amewatoa wasiwasi Watanzania juu ya uvumi wa uwepo wa Ebola Nchini Tanzania ambapo amesema mpaka sasa hakuna yeyote aliyethibitishwa kuwa na Ebola hapa Nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Septemba 14, 2019 Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akiwa na naibu wake, Dk Faustine Ndugulile, mganga mkuu wa Serikali, Profesa Mohamed Kambi na jopo la wataalam wa Shirika la Afya Duniani (WHO), amewataka wananchi kutokuwa na hofu yoyote.
Amebainisha kuwa taarifa za kuwepo kwa ugonjwa huo nchini zimetokana na watu wawili kudhaniwa kuwa na maambukizi ya Ebola katika miji ya Mwanza na Dar es Salaam.
“Hawa walikuwa wahisiwa lakini wizara imefanya vipimo vya maabara zaidi ya mara moja kama inavyoelekezwa na mwongozo wa WHO na kujiridhisha kwamba hawakuwa na maambukizi ya virusi vya ebola hivyo hakuna ugonjwa huo Tanzania,” amesema Waziri Ummy
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment