Search This Blog
Friday, September 27, 2019
Waziri Lugola: Sijawahi kupokea rufaa ya kulalamika kunyimwa kufanya mikutano, Wanakurupuka
Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Kangi Lugola amesema wanaolalamika na kuanza kufanya maandamano na mikutano wanavyotaka wao bila kibali ni lazima wakutane na mkono wa sheria kwani polisi iko imara na hawawezi kuachwa.
amesema Lugola alisema sheria zikifuatwa hakuna shida itakayotokea lakini kinyume na hapo mambo yanakuwa tofauti.
Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo jana baada ya kuzindua ofisi ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) mjini Dodoma.
Alisema sheria inawataka watu wanaotaka kukusanyika kulipa taarifa Jeshi la Polisi, wakiona kimya wanaendelea ila wakipewa barua ya zuio wanatakiwa kusitisha shughuli hizo na kukata rufaa kwa waziri mwenye dhamana ya wizara hiyo.
amesema hajawahi kupokea barua yoyote kutoka chama cha siasa kulalamika kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara au maandamano.
“Tangu nimeteuliwa sijawahi kupokea hata rufaa kulalamika kuwa wamenyimwa haki badala yake wanakurupuka na kulalamika sasa mimi nifanyeje,” amesema Lugola
“Tunao polisi imara, hakuna polisi anayeweza kuwakimbia watu hata kidogo lazima wasonge mbele, sasa hapo ndio mtasikia huyu kaumia au kaumizwa yote ni kwa sababu hawafuati sheria,” alisema Lugola.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment