Search This Blog

Sunday, September 1, 2019

VIDEO: Wanafunzi waililia serikali uchakavu wa majengo


Wanafunzi wa shule ya Msingi Bugururni Kisiwani katika Maspaa ya Ilala jijini Dar es salaam wameiomba serikali kufanya ukarabati wa majengo ambayo yamechakaa na kusababisha kuathiri masomo hasa kipindi cha masika.

Wakizungumza na Muungwana blog wanafunzi wa shule wamesema kuwa hali hiyo imekuwa ikiwaletea usumbufu hususani kipindi cha mvua kwani mapaa ya majengo hayo yametoboka hivyo inaponyesha mvua maji huwamwakia ndani kutokana na kutoboka kwa mapaa ya shule hiyo.

Kwa upande wake mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Philipo Kuzenza amesema kuwa amekuwa akifanya jitihada mbalimbali ikiwemo kutafuta wadau na pia kumwandikia barua Mkurugenzi wa manispaa hiyo ili kukabilia na changamoto hiyo.

''Ni kweli shule yetu imechakaa hasa mapaa kwani inavuja na inaathiri ufundishaji wetu hususani kipindi cha mvua tunapata shida kweli watoto wanakuwa wanavujiwa wakati mwalimu anafundisha hivyo inatuathiri na kupunguza munkali wa walimu kufanya kazi'' amesema Kuzenza

Aidha ameongeza kuwa anaiomba Serikali na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo aione changamoto hiyo ya uchakavu wa majengo na aweze kuishughulikia ili kuondoa kero inayowakabili.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...