Search This Blog
Thursday, September 26, 2019
Serikali Yawaonya Wazazi wanaowafanya watoto wa kike kuwa mitaji
Serikali imewataka wazazi kuacha tabia ya kuwageuza watoto wao hasa wanafunzi wa kike kuwa mitaji ya kipato chao ikiwemo kuwaozesha, na badala yake wawasaidie katika kupata elimu.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha alipokuwa katika ziara ya kikazi wilayani Itilima mkoani Simiyu baada ya kukagua ujenzi wa mabweni ya wasichana shule ya sekondari Nkoma, ofisi ya wathibiti ubora na jengo la veta linaloendelea kujengwa katika kijiji cha Kanadi wilayani humo.
Amewataka wazazi kuwasomesha watoto hao ame ili wawe msaada mkubwa wa baadaye.
Amewataka wazazi kuwekeza zaidi kwenye elimu ili kuwa na mtaji mzuri baadae huku akisisitiza kuwa mtoto wa kike ana haki sawa ya kupata elimu sawa na mtoto wa kiume ambapo katika jamii nyingi bado hazijawapa kipaumbele cha kupata elimu.
"Kuna baadhi ya wazazi bado wanashawishi watoto wao kufanya vibaya katika mitihani yao ya mwisho ili wasiendelee na masomo, niwaombe msishawishi watoto wa kike na kuwatilia vikwazo vya kukatisha masomo mtoto wa kike ana nafasi ya kupata elimu sawa na mtoto wa kiume na pia mtoto wa kike ni wa serikali, hivyo mnaowakatisha masomo mtakiona cha moto,’’ amesema Naibu Waziri Ole Nasha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment