Search This Blog
Wednesday, September 4, 2019
Serikali ya Tanzania yalaani Vurugu za Afrika Kusini dhidi ya Wageni
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamaganda Kabudi amesema vuguvugu linaloendelea nchini Afrika ya Kusini, hatuwezi kulielewa bila kuelewa historia ya nchi hiyo kwa sababu ni kwa kipindi kirefu wananchi wake walinyimwa haki zao chini ya ubaguzi wa rangi.
Ameyasema hayo jana wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika hafla maalumu ya kuwaaga vijana 100, wanaokwenda nchini Israel kwa ajili ya mafunzo ya kilimo kwa vitendo na kusema, Serikali ya Tanzania imeunga mkono kauli ya kulaani vitendo hivyo iliyotolewa na Rais wa nchi hiyo Cyrill Ramaphosa.
''Tanzania inaunga mkono kauli iliyotolewa na Rais wa Afrika ya Kusini Cyrill Ramaphosa ya kulaani vikali na kukemea vitendo hivyo na serikali inaendelea kuwa na mawasiliano ya karibu na Serikali ya Afrika Kusini kwani vuguvugu hizo zimetia doa nchi hiyo'' amesema Profesa Kabudi.
Ikumbukwe hadi sasa vimeripotiwa vifo vya watu takribani watano, huku wengine wakijeruhiwa pamoja na kuharibiwa mali zao, vurugu ambazo zinafanywa na baadhi ya vijana wazawa kwa madai ya kwamba waafrika kutoka nchi zingine wanawachukulia ajira na kazi zao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment