Search This Blog

Thursday, September 19, 2019

Serikali ya Tanzania na Marekani kuendelea kushirikiana katika kupambana na magonjwa


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile jana amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa masuala ya kupambana na magonjwa kutoka Marekani Bw. Robert Redfield.

Mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ofisi ndogo za wizara Jijini Dar Es Salaam yamelenga kuona namna gani nchi hizo mbili zinavyoweza kushirikiana katika kupambana na magonjwa hususani ya kuambukiza na milipuko.

Bwana Redfield amesema ziara yake nchini imekuja mara baada ya kutembelea nchi za Kongo DRC, Rwanda na Uganda ambazo zilikwishapata mlipuko wa ugonjwa Ebola na alitaka kujua Tanzania imejidhatiti vipi kukabiliana na ugonjwa huo usiingie nchini.

Kwa upande wake Naibu Waziri Dkt. Ndugulile amemuhakikishia Mkurugenzi huyo kuwa Tanzania imekuwa ikiwa mikakati ya utayari wa kukabiliana na Ebola hususani mipakani kwa kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa wahudumu wa afya na pia imepeleka vifaa vya uchunguzi vinavyotumika kupima joto la mwili kwa watu wote wanaopita mipakani na kama atashukiwa kuwa na virusi basi kuna vituo maalum vya afya vilivyotengwa kwa ajili ya kutoa matibabu.

Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Muhammad Kambi na Kaimu Mkurugenzi wa Kinga Dkt. Janeth Mghamba kimeondoka na azimio la Serikali ya Tanzania na Marekani kuendelea kushirikiana katika kupambana na kudhibiti magonjwa kupitia program za Global Health Security.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...