Search This Blog
Sunday, September 8, 2019
Polisi wamkamata Mwalimu kwa tuhuma za kumbaka Mwanafunzi wa darasa la saba
Polisi Mkoa wa Mara wanamshikilia Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Bwai A, Wilaya ya Musoma Lazaro Mmanga, kwa tuhuma za kumbaka Mwanafunzi wa darasa la saba mwenye umri wa miaka 14 wakati akijiandaa kufanya mtihani wa Taifa.
Kamanda wa Polisi Mkoa Juma Ndaki amesema Mwalimu huyo alimpitisha Mwanafunzi dirishani na kumuingiza Ofisi ya Mwalimu Mkuu kisha kufunga mlango wa kutokea na yeye akazunguka dirishani na kuingia ndani ya ofisi hiyo.
Amesema baadhi ya Wanafunzi waliokuwa wakimwagilia maua pembeni waliona tukio hilo wakatoa taarifa kwa Viongozi wa Kijiji na Mwalimu akakamatwa akiwa na Mwanafunzi Ofisini na kufikishwa kituoni.
Ndaki amesema baada ya kufikishwa kituoni baadhi ya Wananchi walivamia Kituo hicho kwa lengo la kutaka kumuua na kukazuka vurugu zilizosababisha gari la Polisi kupigwa mawe na kunusurika kuchomwa moto, Watu 42 wanashikiliwa kutokana na vurugu hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment