Search This Blog
Friday, September 27, 2019
Ofisa wa benki CRDB na wenzake watatu kotini kwa utakatishaji wa zaidi ya Sh milioni 100
OFISA wa benki ya CRDB tawi la Ubungo, Andrew Babu (27) na wenzake wafanyabiashara watatu, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam wakikabiliwa tuhuma za Uhujumu Uchumi ikiwamo kula njama, kughushi Tembo kadi, wizi na kutakatisha zaidi ya Sh. Milioni 100.
Mbali na Babu, washtakiwa wengine ni, William Sige (52), Justina Boniphace (49) na Alli Tutupa (35) wote wanaishi jijini Dar es Salaam.
Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mmbando.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon aliwasomea mashtaka yao juzi mahakamani hapo.
Alidai kuwa, kati ya Oktoba 2018 na Aprili 19, mwaka huu washtakiwa wote kwa pamoja walikula njama kutenda kosa la wizi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment