Search This Blog
Wednesday, September 25, 2019
Ngome ya Chadema yazidi kusambaratika Sengerema
Na. James Timber, Mwanza
Aliyekuwa mgombea Udiwani kupitia Chama Cha Chadema Kata ya Chifunfu mwaka 2015 Malebo Ntalano pamoja na Mwenyekiti wa Bawacha, Riziki Juma amekihama chama hicho na kujiunga na CCM na kuisambalatisha ngome hiyo ambayo ilikuwa mwiba kwa CCM.
Amesema kuhama kwake Chadema kumetokana Rais kutimiza waliyokuwa wakiyatafuta wakati wakiwa chadema hivyo hakuna haja yakuwa Chadema tena.
''Nimeondoka Chadema na siludi tena sasa CCM ndiyo sehemu sahihi miradi inatekelezeka alisema Ntalano.
Ntalano alisema.baada ya kuhama yeye amehama na zaidi ya wanachama 30 wa chadema ambao nao wamehamia chamacha mapinduzi.
Kwa upande wake Aliyekuwa mwenyekiti wa Bawacha kata ya Chifunfu Riziki Juma alisema kuwa kuhamia kwake CCM alichagua mahali.salama na penye heshima hivyo atafanya kazi kwa Uhuru na amani.
Katibu wa CCM tawi la Chifunfu Julias Mngele amekili kuwapokea wanachama hao na kukili wazi kuwa kuhama kwao CCM kumewapunguzia kazi kwenye uchaguzi bwa serikali za mitaa kwa kuwa wao walikuwa ni kikwazo Cha ushindi wa CCM.
Viongozi mbalimbali na wanachama wa Chadema wamekuwa. wakikihama chama hicho na kujiunga na CCM akiwemo diwani wa Kata ya Nyampulukano Emmanuel Munwazi na chama hicho kuwa kimekosa nguvu wilayani.sengerema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment