Search This Blog

Sunday, September 15, 2019

Mwanariadha wa Kenya aweka rekodi mpya ya dunia


Mwanariadha kutoka nchini Kenya, Geoffrey Kamworor amevunja rekodi ya dunia katika mbio ndefu za Copenhagen Half Marathon, zilizofanyika jana Jumapili nchini Denmark.

Kwenye mbio hizo za kilometa 21, Kamworor alitumia muda wa dakika 57:01. Na kuweka rekodi mpya ya kutumia muda mfupi zaidi wa Half Marathon duniani.

Kamworor ambaye ni bingwa mara tatu wa mbio hizo, Amevunja rekodi ya Mkenya mwenzie, Abraham Kiptum ya kukimbia umbali huo kwa dakika 58.01, Ambayo aliiweka katika mbio za Valencia Half Marathon mwezi Oktoba mwaka jana.

Tayari shirikisho la riadha ulimwenguni (IAAF). Limeiweka rekodi hiyo mpya ambayo ilikuwa inashikiliwa na Abraham Kiptum kwa muda wa dakika 58:18.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...