Search This Blog
Sunday, September 29, 2019
Mtalii afariki akiruka kwa Parachuti Mlima Kilimanjaro
Mtalii raia wa Canada, Justin Kyllo (51) amefariki baada ya Parachuti alilokuwa akitumia kuruka angani kutoka kilele cha mlima Kilimanjaro nchini Tanzania kugoma kufunguka.
Kamishna msaidizi mwandamizi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Pascal Shelutete amethibitisha kifo cha mtalii huyo, kwamba kimetokea katika kituo cha Stella Point kilichopo katika mlima huo.
Amesema mtalii huyo alifika Septemba 20 mwaka huu kwa ajili ya kupanda mlima, leo asubuhi alitumia Parachuti kwa ajili ya kuruka angani ili kushuka chini ya mlima lakini iligoma kufunguka na kusababisha kifo chake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment