Search This Blog

Tuesday, September 17, 2019

Kocha Julio Amkana Manula Mbele ya Kaseja...Manula Inabidi Apambane


Mchezaji wa zamani wa klabu ya Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema kuwa anakubaliana na maamuzi ya Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Ettiene Ndayiragije kutomjumuisha golikipa Aishi Manula kwenye kikosi cha Taifa Stars.


Julio amesema kuwa uamuzi huo ni sahihi kwakuwa golikipa namba moja wa sasa wa Taifa Stars, Juma Kaseja ni mzoefu kuliko Manula.

"Unajua Kaseja ana uzoefu mkubwa kuliko Manula, kwangu Manula kuachwa Stars ni maamuzi sahihi kwa Kocha. Anapaswa kukaa chini na kujitafakari amekosea wapi na pia ajifunze kutoka kwa Kaseja namna alivyopambana mpaka kufika hapo alipo", amesema Julio.

Ikumbukwe kuwa hii ni mara ya pili kwa Manula kutojumuishwa katika kikosi, ambapo mara ya kwanza aliachwa katika mchezo dhidi ya Kenya pamoja na mchezo dhidi ya Burundi, na sasa ameachwa katika kikosi kinachojiandaa katika mchezo dhidi ya Sudan.

Julio ambaye hivi sasa ameachana na kazi ya kufundisha soka kwa muda, baada ya kupitia klabu kadhaa kama kocha ikiwemo Simba, Mwadui FC na Dodoma FC.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...