Search This Blog
Thursday, September 19, 2019
Katibu Mkuu Wizara ya Afya azungumza na Wabunge wanaopambana na Malaria kutoka Uingereza na Ujerumani
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula amekutana na kufanya majadiliano na Chama cha cha Wabunge wanaopambana na Malaria kutoka Uingereza na Ujerumani pamoja na Wabunge wa Tanzania wa Chama cha kupambana na Malaria na Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele(TAPAMA) pamoja na Watendaji kutoka Wizara ya Afya na TAMISEMI.
Katika majadiliano hayo wamekubaliana kushirikiana katika kutokomeza magonjwa hayo hapa nchini ili kuweza kuokoa maisha ya wananchi hususan watoto wadogo.
Kwa upande wa Malaria kulingana na mkakati wa mwaka.2015-2020 ulikua na lengo la kupunguza Malaria chini ya asilimia 5 mwaka 2016 na baada ya tathimini wamefanikiwa kupunguza hadi kufikia asilimia 7.3 ikiwa ni lengo la.kufikia asilimia moja mwaka 2020 hivyo wameainisha na kupanga mikakati ya kutokomeza kwa asilimia hiyo.
Na upande wa Magonjwa yaliyokuwa.hayapewi kipaumbele(NTD),Wizara imejikita katika kudhibiti magonjwa matano ikiwemo usubi,minyoo,trakoma,kichocho pamoja na matende na mabusha.
Kwa mwaka huu wamefanikiwa kufanya upasuaji wa mabusha kwa watu 1607 na watu 16748 wameweza kurekebishiwa vikope na kuendelea kuona na hivyo kubakiza kuwafikia watu 5923 ambao kwa namna moja hawakuweza kujitokeza kutokana na imani potovu hata hivyo wizara kwa kushirikiana na mpango wa taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele wanaendelea kufanya uhamasishaji kupitia vyombo vya habari pamoja na kugawa dawa kwa wananchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment