Search This Blog
Tuesday, September 3, 2019
Kagera waelekezwa jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa Ebola
Timu za uendeshaji huduma za Afya za Halmashauri (CHMTs) za Mkoa wa Kagera zimeelekezwa jinsi ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Ebola, ikiwa ni moja kati ya mikakati ya Serikali kuwakinga Watumishi wa Sekta ya Afya endapo utaingia nchini.
Hayo yamejiri wakati wa mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kuzingatia taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC Standard) inayoendelea Mkoani Kagera ikiwa ni moja kati ya mikoa iliyo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola.
Katika Mafunzo hayo, Afisa kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Wizara ya Afya Dkt. Alex Sanga amesema kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo zipo katika hatari ya kupata wagonjwa wa Ebola kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu na ukaribu na Nchi ya Uganda na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ambazo tayari zimekwishapata janga hilo.
Dkt. Sanga amesema kuwa, taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinasema kuwa takribani zaidi ya Wagonjwa 2950 wamethibitika kuwa na Ugonjwa wa Ebola, huku zaidi ya Wagonjwa 2000 wakipoteza maisha tokea mlipuko huo ulipojitokeza Agosti 2018, huku Wataalamu wa Afya 131 walipata maambukizi, ambapo 41 kati yao wamepoteza maisha
Aidha, Sanga amesema kuwa Serikali ya Tanzania imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha utayari wa kukabiliana na tishio la Ugonjwa huo ili kuhakikisha hauingii nchini, ikiwemo kuelimisha jamii njia za kujikinga na Ugonjwa ili kuzuia usiingie nchini, na kutoa Elimu kwa Watoa huduma za Afya juu ya kumuhudumia mtu mwenye dalili za Ebola endapo atatokea.
Hata hivyo, Dkt. Sanga amesema kuwa, Shirika la Afya Duniani (WHO) inakusudia kuzuia Ugonjwa wa Ebola kwa kuimarisha huduma za uchunguzi na kusaidia nchi zilizo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...



No comments:
Post a Comment