Search This Blog

Sunday, September 1, 2019

Bilioni mbili zahitajika kujenga hospitali ya kisasa Babati


Na John Walter-Babati-Manyara

Ili kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi, Hospitali ya mji wa Babati mkoani Manyara inahitaji shilingi bilioni mbili kukamilisha mradi wa  Master Plan itakayowezesha Hospitali hiyo iwe katika mwonekano wa  kisasa.

Hospitali hiyo ya mji wa Babati maarufu Mrara ilianza mwaka 1956 kama zahanati na baadaye wakaongeza majengo ikawa kituo cha afya kisha kuwa Hospitali bila kuwa na ramani kamili.

Kaimu mganga Mkuu Hospitali ya mji wa Babati (MRARA) Dr. Pastory Mahendeka ameileza kamati ya Siasa ya Mji wa Babati iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Ccm mkoa wa Manyara Saimon Lulu,kwamba tayari master Plan hiyo imefikishwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kinachosubiriwa kwa sasa ni kibali ili ujenzi huo uanze kwa kiasi cha fedha walizonazo kwa sasa.

Pamoja na hayo,Dr.Mahendeka ameiomba serikali itoe kibali cha kuajiri watumishi katika Hospitali hiyo kwa kuwa kuna upungufu wa asilimia 48 ya watumishi ambao wanazidiwa na majukumu.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Manyara Mheshimiwa Saimon Lulu, amepongeza hatua hiyo na kuahidi kuhimiza serikali na wadau mbalimbali ili kuweza kufanikisha jambo hilo muhimu.


Hopitali ya Mji wa Babati MRARA ni Muhimu kuboreshwa kwani  licha ya kuwa ni ya mji lakini pia inahudumia wakazi wa wilaya za Mbulu,Hanang,Simanjiro,Kiteto,na mikoa ya Arusha na Dodoma haswa wilaya ya Kondoa.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...