Search This Blog
Wednesday, August 28, 2019
Wizara ya Afya yaja na mfumo wa Dharura na Uokozi
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara nchini TANROADS iko mbioni kuanzisha mfumo wa huduma za dharura na uokoaji katika barabara kuu nchini.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa lengo namba tatu (AFYA BORA NA USTAWI) kati ya malengo 17 ya Malengo Endelevu ya Maendeleo (SDG’s) kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Kwenye ukumbi wa mikutano bungeni Jijini Dodoma.
Waziri Ummy Mwalimu amesema, “Mfumo huu una lengo la kusaidia kupambana na dharura au maafa pindi yanapotokea na kuweza kusaidia upatikanaji wa huduma kwa haraka na tutaanza na vituo 7 vya huduma za dharura katika barabara kuu toka Mkoa wa Dar Es Salaam mpaka Ruaha Mbuyuni Mkoa wa Iringa".
Amevitaja vituo vya huduma za dharura ambayo vitaanzishwa kuwa ni Kituo cha Afya Kimara (DSM), Hospitali ya Tumbi, Kituo cha Afya Chalinze (PWANI), Zahanati ya Fulwe (Mikese Morogoro), Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Hospitali ya St. Kizito (Mikumi, Morogoro) pamoja na Zahanati ya Ruaha Mbuyuni Darajani (Iringa).
"Tumeweza kununua gari za kubebea wagonjwa (Ambulance) 12 ambazo tutazisamba katika vituo vya huduma za dharura” amesema Waziri Ummy na kuendelea “bado tuna lengo la kuongeza magari matatu ya uzimaji moto yenye uwezo wa kuinua na kukata vyuma ili kuwaokoa majeruhi na kuwapatia huduma eneo la tukio
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment