Search This Blog
Thursday, August 8, 2019
SIDO wafanikiwa kutengeneza Mashine ya kisasa ya kukata Nyama
Na. John Walter, Arusha
Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Arusha kupitia kituo chao cha uendelezaji wa Biashara Wamefanikiwa kutengeneza mashine ya kisasa ya kukata nyama itakayokuwa Mbadala wa Matumizi ya Magogo.
Hayo yamesemwa na Meneja wa SIDO mkoani hapo Nina Nchimbi wakati wa akizungumza na Muungwana Blog kwenye maonyesho ya 26 ya Kilimo na Mifugo (Nane nane) Njiro Jijini Arusha, ambapo amesema mashine hizo wataziuza kwa wafanyabiashara wa nyama kwenye mabucha kwa bei nafuu ili kila mmoja awe nayo.
Amesema wameamua kutengeneza mashine hiyo kwa kuwa Bodi ya nyama nchini imeshapiga marufuku kukata nyama kwenye Magogo ifikapo Septemba 30 mwaka huu.
Nchimbi amesema wapo tayari kuwahudumia wajasiriamali kwa kuwapatia kuwajengea uwezo ili waweze kuanzisha viwanda na kuzalisha bidhaa bora na sahihi kwa mlaji wa Mwisho.
Mbali na hayo, SIDO wameiomba serikali kwa kushirikia na shirika hilo ambalo lipo kila mkoa kutenga maeneo kwa ajili wajasiriamali kwenye halmashauri zote kwa kuwa wapo wajasiriamali wengi lakini wanakabiliwa na uhaba wa maeneo ya kufanyia shuguli zao hali inayowafanya wengine kufanyaia kazi maeneo ambayo sio rafiki.
Kauli mbiu Nane nane mwaka 2019: “Kilimo,Mifugo na Uvuvi kwa Ukuaji wa Uchumi wa Nchi.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment