Search This Blog
Sunday, August 4, 2019
Nkurunziza ashinda mbio za baiskeli za Tour de Kigali
Mwendesha baiskeli wa Rwanda Yves Nkurunziza Jumamosi alishinda sehemu ya pili ya Kombe la mbio za Baiskeli 'Tour de Kigali' la mwaka 2019 ambalo limeshuhudia waendesha baiskeli wakishindana katika mji wa Kigali.
Mbio hizo ni makala ya pili baada ya mbio za 'Northern Challenge' zilizofanyika mwezi uliopita ikiwa ni sehemu ya Kombe la mbio za Baiskeli la Rwanda.
Washindani walianza mbio zao huko Intwari, Nyamirambo, na kupita Nyakabanda, Kimisagara, Nyabugogo, Muhima, Yamaha, APA COPE, Gakiriro hadi Gitega. Katika kitengo cha vijana "junior category" Jeremy Ngendahayo alishinda mbio kwa kutumia saa 2 na sekunde 39, akifuatiwa na Elysee Bikorikana aliyetumia saa 2 dakika 44 na sekunde 32 seconds na Jean-Nepo Bigirimana akawa wa watatu kwa kutumia saa 2 dakika 44 na sekunde 51.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment