Search This Blog
Thursday, August 1, 2019
Mwanafunzi ajirusha kutoka kwenye ndege ikiwa angani na kufariki
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cambridge, Uingereza, Alana Cutland amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka katika ndege umbali wa futi 5000 angani.
Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 19 inadaiwa alilazimisha kufungua mlango wa ndege hiyo kisha kujirusha katika eneo la Anjajavy.
Polisi nchini Madagasca wamedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa kwa sasa wanaangalia nini kilitokea sekunde chache kabla ya msichana huyo kufa.
Mkuu wa Polisi wa Madagasca, Sinola Nomenjahary alisema kuwa taarifa za awali zinaonyesha kwamba rafiki wa karibu wa msichana huyo, Ruth Johnson na rubani wa ndege hiyo walijaribu kumzuia kwa kumshika mguu kwa sekunde kadhaa bila mafanikio.
Msichana huyo ambaye alikuwa mwaka wa pili katika masomo ya Biolojia alikuwa akisafiri kwenda nchini India kwa ajili ya safari ya kimasomo ambako inadaiwa walibakiza dakika 10 pekee kutua.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment