Search This Blog
Monday, August 19, 2019
Mkazi wa Tandale Afikishwa Mahakamani kwa Kumkata Mwanamke Bikra yake kwa Kiwembe
Mkazi wa Tandale kwa Mtogole jijini Dar es Salaam, Siasa Samwel (30), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa kosa la kumjeruhi kwa kumkata kwa viwembe sehemu za siri, Zaina Issah.
Mtuhumiwa huyo anadaiwa kumkata mwanamke huyo sehemu za siri Novemba 15, mwaka jana na kumsababishia kupoteza bikra yake.
Akisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Boniface Lihamwike na Mwendesha Mashtaka wa Serikali Veronica Mtafya, amedai tukio hilo lilitokea eneo la Tandale Chama Wilayani Kinondoni jijini Dar es salaam.
Hata hivyo, mshtakiwa huyo amekana shtaka hilo ambapo mwendesha mashtaka alidai upelelezi haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kusomwa kesi hiyo.
Hakimu Lihamwike amesema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu wenye barua za utambulisho, nakala ya vitambulisho na kusaini bondi ya Sh milioni moja.
Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya hayo na kurudishwa rumande hadi kesi yake itakapokuja kusomwa tena Septemba 2, mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment