Search This Blog
Tuesday, August 27, 2019
Majeruhi kuwaweka nje ya uwanja Kylian Mbappe na Cavani
Mshambuliaji nyota wa Paris Saint Germain, Kylian Mbappe atakuwa nje ya uwanja kwa wiki nne na mwenzake Edinson Cavani kwa wiki tatu baada ya wawili hao kuumia uwanjani katika mechi ya ligi kuu ya Ufaransa (Ligue 1) dhidi ya Toulouse.
Mbappe aliyekuwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kilichotwaa ubingwa wa dunia, alitoka baada ya kuumia misuli ya mguu wa kushoto wakati akichanja mbuga kwenye mechi hiyo ambayo PSG iliibuka na ushindi wa goli 4-0 kwenye uwanja wa Parc des Princes.
Mbappe huenda akakosa mechi ya ligi ya mabingwa Ulaya iliyopangwa kupigwa Septemba 17 au 18. Pia atakosa mechi tatu za ligi pamoja na mechi za Ufaransa michuano ya awali ya mataifa ya Ulaya, Euro 2020 dhidi ya Albania na Andorra zitakazofanyika Ufaransa mwezi ujao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment