Search This Blog
Monday, August 19, 2019
Maalim Seif atema cheche asema hakuna wa kumziba mdomo
Mshauri Mkuu wa chama cha upinzani cha ACT- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amesema hakuna mtu anayeweza kumziba mdomo wakati akikemea maovu.
Maalim Seif amesema yeye ni mpinzani, hivyo anawajibu wa kukosoa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Akizungumza Mjini Unguja wakati wa uzinduzi wa uchaguzi wa ngome ya wanawake wa chama hicho katika Ofisi ya ACT- Wazalendo, Bububu, mkoa wa Mjini Magharibi alisema atazungumza bila kumuogopa yoyote.
Aidha, amesema kuwa imekuwa ni kawaida kwa Jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya chama hata ile ya ndani ambayo inafanyika kisheria.
Alisema yanayofanyika yanalengo la kutaka kuwarudisha nyuma harakati za kisiasa za chama chao “Nasema hatutakubali kamwe kurudishwa nyuma,”amesema Maalim Seif
Maalim Seif ametoa kauli hiyo mara baada ya kuzuiwa kufanya mikutano katika ukumbi ambao wamekuwa wakifanya mikutano yao ya ndani kwa madai ya kupata vitisho ikiwemo kufungiwa kumbi zao.
Hata hivyo, ameongeza kuwa kumekuwa na visingizio vya kila aina kila wanapokwenda kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kwa ajili ya kufanya shughuli zao za kisiasa, kwani wamekuwa wakihangaishwa kwa lengo la kuzuia shughuli zao ambazo zipo kwa mujibu wa sheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment