Search This Blog
Thursday, August 22, 2019
Maafisa elimu nchini watakiwa kufanyakazi kwa ushirikiano
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu Tixon Nzunda amewaagiza Maafisa elimu Maalum na watu wazima kufanyakazi kwa ushirikiano ili kuendana na dira ya nchi inayotaka kuandaa jamii ya watu walioelimika wenye maarifa na ujuzi.
Ameyasema hayo wakati akifunga Kikao kazi cha Maafisa elimu Mkoa, Maafisa elimu Maalum na Maafisa Elimu watu wazima, kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango, Jijini Dodoma.
Nzunda amesema kuwa hatuwezi kujenga nchi yenye uchumi wa viwanda na watu wanaoweza kushindana bila kuwa na watu wenye maarifa sahihi, ujuzi kamili, kujiamini, wazalendo na wanaoipenda nchi yao kwa ajili ya kuleta mabadiliko ya kweli na maendeleo katika mapinduzi ya viwanda.
Amesema Sekta ya elimu ni kubwa hivyo amewaomba kujenga mshikamano, kufanyakazi kama timu na kusaidiana kwa hali na mali ili kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu kwa kuisaidia jamii kuona umuhimu wa elimu nchini
“Acheni majungu mafanikio ya idara yawe ni ya kila mmoja, msitengeneze makundi ndani ya Idara na ndani ya sekta kwa kuwa sekta ya elimu ni mafanikio ya Taifa, watu walioelimuka, wanaojiamini wenye maarifa, ujuzi na wanaoweza kujiamini,” anasisitiza Nzunda
Amesema kuwa katika kuleta maendeleo ya elimu nchini ni lazima kufanyakazi kwa umoja na upendo kwani bila kufanya hivyo hakutakuwa na mabadiliko na kutarudisha nyuma juhudi za Serikali katika kuleta maendeleo kwa jamii na kupunguza changamoto katika sekta ya elimu nchini.
Amewataka Maafisa elimu nchini kuhakikisha wanasimamia taaluma kuanzia ngazi ya awali, msingi, sekondari na watu wenye mahitaji maalum kwa kusimia mitaala wa elimu nchini na kuhakikisha maafisa elimu kata wanatimiza majukumu yao kikamilifu ili kuimarisha elimu kuanzia ngazi ya awali.
Aidha amewataka kuhakikisha wanasimamia utendaji kazi wa watumishi, utunzaji wa siri na uwajibikaji ili kujenga nidhamu kwa watu tunaowasimamia .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment