Search This Blog

Monday, August 12, 2019

Lori lingine la mafuta lateketea kwa moto

Lori  jingine la mafuta aina ya Scania, lenye namba ya usajili T 243 BCU, na tela T 685 DCV mali ya kampuni ya Njombe Filling Station, limeteketea kwa moto baada ya kupata ajali katika Kijiji cha Ngadinda Halmashauri ya Madaba, Ruvuma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma (RPC), Simon Maigwa Marwa, amethibitisha tukio hilo.

“Tukio la ajali ni kweli limetokea jana saa nne usiku (kuamkia leo Jumatatu) Songea Vijijini ambapo lori lilikuwa limebeba shehena petroli na likiendeshwa na Hubert Mpete ambaye bado hajajulikana alipo.  Lori hilo liliacha njia na kuingia porini kisha kugonga mti na kuwaka moto,  na kichwa (cabin) kiliungua chote,” alisema Marwa.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...