Search This Blog
Monday, August 19, 2019
Kisa wizi apewa adhabu ya kunywa ndoo mbili za maziwa
Wizi si jambo zuri hata kidogo. Ndiyo sio jambo zuri kwa sababu hurudisha nyuma maendeleo ya watu. Kuna nyakati mtu anakuwa na mali zake ambazo ameitafuta kwa tabu sana lakini mtu mmoja au kundi la watu kadhaa linaweza kumtia umasikini ndani ya muda mfupi sana.
Mara nyingi tumezoea kuona mwizi akikamatwa na watu kwenye jamii mbalimbali, watu hujichukulia hatua mkononi ama kwa kumuua kwa njia mbalimbali kama kumchoma moto au kumkata kwa vitu vyenye ncha kali kama vile panga na kadhalika
Sasa jana mkoani Iringa kuna mwizi amepewa adhabu kulingana na alichoiba. Inaelezwa aliiba ndoo mbili za maziwa zenye ujazo wa lita 20 na alipokamatwa akapewa adhabu ya kunywa na kumaliza maziwa yote yaliyomo kwenye ndoo zote mbili.
Said Kione anaesadikiwa kuiba ndoo mbili za lita 20, za maziwa fresh jana eneo la Miyomboni, Iringa amepewa adhabu ya kunywa ndoo zote mbili za maziwa aliyoiba badala ya kupelekwa polisi baada ya kudai kuwa alilazimika kuiba kutokana na njaa na hamu ya maziwa hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment